AGAPE SINGERS

Friday 16 August 2013

MADHABAU vs MIMBARI: Quoted from MC

Madhabahu ni mahali pa kutolea kafara  au uvumba.
"Nuhu akamjengea bwana madhabahu;akatwa katika kila mnyama aliye safi na katika kila ndege aliye safi,akavitoa sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu."(Mwanzo 8:20)
"Kisha kuhani atatia baadhi ya hiyo damu juu ya kila pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba mzuri mbele ya Bwana iliyo ndani ya hema ya kukutania;kisha damu yote ya huyo ng'ombe ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa iliyoko mlangoni pa hema la kukutania. "(Lawi 4:7)
Mtu yeyote akitaka kufanya kazi ya Madhabhu bila kuwa nasaba ya Haruni anatafuta kifo,hivyo kuhani alikuwa anateuliwa na Mungu mwenyewe kwa jili ya kazi yake takatifu na ndiye pekee aliyeruhusiwa kufika madhabahuni pa Bwana.
"Nawe na wanao pamoja nawe mtautunza ukuhani wenu,kwa ajili ya kila kitu cha madhabahu na kwa ajili ya vile vilivyomo ndani ya pazia nanyi mtatumika.Nawapeni ukuhani kuwa utumishi wa kipawa;na mgeni akaribiaye atauawa".(Hesabu 18:7)

"Lakini alipokuwa na nguvu moyo wake ulitukuka,hata akafanya maovu akamwasi Bwana,Mungu wake;kwani aliingia hekaluni mwa Bwana ili afukizeuvumba juu ya madhabahu ya kufukizia.Azaria kuhani akaingia nyuma yake na pamoja naye makuhani themanini wa Bwana,mashujaa;wakamzuia Uzia mfalme,wakamwambia,si haki yako Uzia kumfukizia Bwana uvumba,ila ni haki ya makuhani wana wa Haruni,waliofanywa wakfu ili wafukize uvumba toka katika patakatifu;kwa kuwa umekosa;wala haitakuwa kwa heshima yako kutoka kwa Bwana,Mungu.Akaghadhibika Uzia;naye alikuwa na chetezo mkononi cha kufukuzia uvumba;naye hapo alipowaghadhibikia makuhani,ukamtokea ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani nyumbani mwa Bwana karibu na madhabahu ya kufukizia."(2Nyakati 26:16-19)
Hivyo katika madhabahu maungamo ya dhambi za watu yanafanywa na kuhani(walawi 8:14-16;Hesabu 28,29)
Mimbari ni  jukwaa au mahali pa kusimama juu yake ili kuonekana.
Mungu anazungumza na watu kupitia watumishi wake-torati inasomwa.
"Naye Ezra kuhani,akasimama juu ya mimbari ya mti,waliyokuwa wameifanya kwa kusudi hilo;na karibu naye wakasimama matithia na Shema,na Anayo,na Uria,na Hilkia,na Maaseya,mkono wake wa kuume,na mkono wake wa kushoto,Pedaya na Misbael,na Malkiya,na Hashumu,na Hashbadani na Zekaria,na Meshulamu.Ezra akakifunua Kitabu machoni pa watu wote;(maana alikuwa juu ya watu wote);na hapo alipokifungua,watu wote walisimama;Ezra akamhimidi Bwana Mungu mkuu.Nao watu wote wakaitika amina amina,pamoja na kuinua mikono yao;kisha wakainama vichwa vyao,wakamsujudu Bwana kifudifudi."(nehemia 8:2,4,5)
"Kwa maana tangu zamani za kale musa anao watu wahubirio mambo yake;katika kila mji husoma kila sabato katika masinagogi."(Mdo.15:21)
"Kisha,baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii,wakuu wa sinagogi wakatuma mtu kwao,na kuwaambia,Ndugu,kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa,lisemeni."(Mdo.13:15)
zoezi la kuendesha ibada kwa jinsi hii iliendelea kizazi hadi kizazi toka Adamu hadi Yakobo-Mungu alichagua wanaume wasogeze sadaka za kafara mbele za Bwana.Wanaume hawa hawakuwa Walawimaana Kabila la Lawi halikuwepo.Muda ulipofika ;kulingana na ratiba yake,aliacha ukuhani wa wazao wa kwanza na kuchagua walawi.
Mungu alidhihirisha hili alipochagua walawi"Mimi tazama nimewatwaa walawi na kuwatoa kati ya wana wa Israeli badala ya wazaliwa wa kwanza wote wafunguao tumbo katika wana wa Israeli;na hao walawi watakuwa wangu."(Hes.3:12)
Roho ya unabii inasemaje?
"Wakati sauti ya kilio imekwisha"iliposikika kutoka mdomoni mwa Kristo ilikuwa wakati wa kutoa dhabihu ya jioni,kondoo anayemwakilisha Kristo alikuwa ameletwa kuchinjwa,kuhani akisimama na kisu hali watu wakiangalia,lakini nchi ilitetemeka kwa sababu Bwana mwenyewe alikaribia karibu,kwa sauti ya mpasuko,pazia la hekalu likapasuliwa kwa mkono usioonekana vipande toka juu hata chini,na kukifungua wazi kwa macho ya watu kuona chumba cha patakatifu palipokuwa pakijaa utukufu wa Mungu.Mahali patakatifu mno pa hekalu la duniani hapakuwa patakatifu tena."[1]Ellen G.White,Tumaini la Vizazi Vyote(Harare,Zimbabwe,Eastern africa Division Publishing Association,2001),p428-429
Sasa bila ubaguz;paulo anasema:
".....sisi sote(wanaume na wanawake)tumepata njia ya kumkaribia baba katika Roho."(Efeso.2:18)
Kanuni ni ile ile;Mungu ndiye mteuzi wa nani atumike kama kuhani :
Kuhani mkuu:"Hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii,ila yeye aitwaye na Mungu kama vile Haruni,Hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu,lakini yeye aliyemwambia ndiwe mwanangu,mimi nimekuzaa,kama asemavyo mahali pengine,ndiwe kuhani kwa mfano wa melkizedeki"(Waeb.5:4-6).
"Bali ninyi ni mzao mteule,ukuhani wa kifalme,taifa takatifu,watu wa milki ya Mungu,mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu"(1Petro 2:9)

No comments: