AGAPE SINGERS

Wednesday 16 July 2014

Bwana Yesu Asifiwe!!

Tunaendelea tena leo kukuletea mfululizo wa nguvu zilizomo na 

uwezo uliomo katika Damu ya Yesu Kristo.

Mathayo 27:29 inatuambia ya kuwa Yesu alivikwa “taji ya miiba” 

kichwani pake; na “wakamdhihaki, wakisema, salamu, Mfalme wa 

Wayahudi”.

 
Waliomsulubisha walipokuwa wanamdhihaki katika tendo hilo, 

hawakujua kwa Damu ya Yesu iliyomwagika wakati huo, ilikuwa 

inaandaa mazingira ya watakaomwamini kufanyika wafalme!
 

Hii ni kwa sababu “taji” ni sehemu ya vazi la kifalme! Ufunuo wa 

Yohana 5:9,10 inatuambia ya kuwa juu ya Yesu: “Ukamnunulia 

Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na 

taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu, nao 

wanamiliki juu ya nchi”.
 

Tafsiri za biblia za kiingereza zinasema “Ukawafanya wafalme na 

makuhani kwa Mungu wetu, nao wanamiliki juu ya nchi”. Kwa hiyo, 

kama unamwamini Yesu na umeokoka, umefanyika mfalme katika 

Yeye. Je, unalijua hili? Na je, unaliamini kwa kiwango kipi? Je, 

unajua kuishi na kutawala kama mfalme katika ulimwengu huu 

maana yake nini? (Warumi 5:17).

No comments: