AGAPE SINGERS

Wednesday 23 July 2014

NENO ZITO

Si kila aliyefanikiwa kimaisha ni fisadi’

Mkuu wa Kanisa la Wasabato Kanda ya Mashariki, Mchungaji Marko Marekana, amekemea tabia ya baadhi ya watu kulalamikia maisha bora bila kujishughulisha na kuwaita wenzao waliofanikiwa mafasadi na badala yake amewataka kufanyakazi kwa bidii na maarifa kujiletea maendeleo.

Mchungaji huyo pia amekea tabia ambayo amesema kuwa inazidi kuenea miongoni mwa watu ya kuwaita wenzao ambao Mungu amewajalia kupata uwezo kifedha kwamba mafisadi ama Freemansons.

Alisema hayo juzi kwenye viwanja vya Biafra Kinondoni, jijini Dar es Salaama, ambako kunafanyika mikutano ya injili ya kimataifa iliyopewa jina la Mwayachunguza Maandiko.


Kauli ya Mchungaji huyo ilikuja kufuatia wingi wa watu wanaohudhuria mikutano hiyo ambao wamekuwa wakisimama juani kutokana na kuwepo kwa mahema machache na hivyo kuleta usumbufu.

"Hali hii ya baadhi ya wengine kukaa ama kusimama juani siyo nzuri, hivyo ninawaomba wazee wa Dar es Salaam kukutana kutafuta uwezekano wa kupata mahema zaidi ili watu wote wakae kwenye kivuli," alisema na kuendelea:

"Lakini wapo watu wenye uwezo wa kusaidia mikutano hii lakini wameniambia kuwa wanahofia kuitwa mafisadi na siyo jina hilo kuna lingine la Freemansons, siyo kila mtu ambaye amefanikiwa kifedha ni fisadi'.

Alisema wapo watu ambao Mungu amewajalia kwa shughuli zao kihalali wakisafiri ndani na nje ya nchi kuleta biashara zao, lakini wanaitwa mafisadi ambapo amekea hali hiyo.

Mchungaji Marekana aliwakumbhusha waumini kuwa kumtegemea Mungu siyo lazima muumini awe na maisha duni, hivyo akawahimiza kufanya kazi na siyo kumwona kila aliyefanikiwa kimaisha kuwa ni fisadi.

"Maisha bora hayawezi kuja kwa kushinda kwenye bao, karata ama pool, kila mtu anatakiwa kufanya kazi, hivyo acheni tabia ya kuwaita wenzenu mafisadi huku nyie hamfanyi kazi," alisema Mchungaji Marekana.

Mikutano hiyo ambayo inashirikisha makanisa yote ya Wasabato ya jijini Dar es Salaam inaendeshwa na wachungaji
Baraka Muganda na Geofrey Mbwana kutoka makao makuu ya kanisa hilo nchini Marekani.

Mbali na hao pia wapo wana chuo kutoka Washington Adventist University, Marekani, pamoja na kwaya maarufu ya  Ambassador of Christ kutoka kanisa la Wasabato la Remera, Kigali, nchini Rwanda.
 

No comments: