SAFARI YENYE MATUMAINI
"Safari Yenye Matumaini"
Na Elias Wankyo
Isaya
43:18 "Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya
zamani. Tazama, nitatenda neno (jambo) jipya" "Nitafanya njia hata
jangwani, na mito ya maji nyikani."
New
King James Version. Isaiah 43:18,19 "Do not remember the former things,
nor consider the things of old. Behold, I will do a new thing" "I will
even make a road in the wilderness and rivers in the desert."
Katika
nchi ya Colombia kule Amerika ya Kusini mwanamke mmoja aitwaye Ingrid
Betancourt aliamua kugombea Uraisi wa nchi hiyo. Katika mojawapo ya
kampeni zake alitekwa nyara na kundi moja la ugaidi nchini humo. Kwa
hali ngumu na ya kusikitisha alichukuliwa mateka na baadhi ya watu wa kundi lake
na wakafichwa kwa muda wa miaka sita. Lakini mwaka 2008 mwishoni,
Majeshi ya Serikali ya Colombia yalivamia maghaidi hao na kumkomboa
Ingrid na watu wake wote wakiwa hai.
Ingrid
aliporudi nyumbani salama alilakiwa na watu wakiwemo ndugu na jamaa
zake. Ingrid akaenda mara moja kwa mama yake akamkumbatia kwa furaha
iliyo kuu, na mbele ya waandishi wa habari akasema maneno haya mazito
ambayo niliyaandika kuwa kumbukumbu nilipoyasikia kwenye taarifa ya
habari:"Don't cry for me now. You don't have to cry for me anymore". Kwa
Ingrid, inaonekana alikuwa tayari kufunga kitabu cha historia ya miaka 6
alipokuwa mateka, na kwa vile alikuwa huru sasa, alimwambia mama yake
na watu wake, sasa kulia kwa ajili yake kungefikia mwisho, wafunge
kitabu hicho kabisa, waanze maisha upya na waendelee na "Kitabu" kipya
cha maisha.
1)
Safari yenye matumaini inahitaji tusiwe watumwa (au kufungwa kama tuko
jela) kwa uzoefu au mambo mabaya katika maisha yetu yaliyokwishapita.
(Not to be prisoners of our negative "experiences" in the past).
Kila
mwanadamu katika maisha amepitia hali fulani ngumu katika maisha, ila
hali hizo zinatofautiana kati ya mtu na mtu. Kuna wengine ambao uzoefu
au hali waliyopitia ni ngumu sana na imesababisha majeraha na makovu
makubwa. Kwa sisi Waadventista tukikutana kanisani siku ya Sabato, hasa
makanisa ya mijini, tumekuwa tumevaa vizuri, na kawaida tukiulizana,
"habari gani?" Jibu la rahisi huwa kwa kawaida, "Ni nzuri". Lakini kwa
ujumla tunaweza tusijue watu wanayopitia katikati ya wiki, au kwa ujumla
katika maisha yao.
Nilikuwa
katika mahubiri ya hadhara (Public Evangelism), Mhubiri alipotoa wito,
nikashuka jukwaani, kuwapa mkono na kuwakaribisha walioitikia wito. Mama
mmoja akasogea mbele akiwa na mnyororo mkubwa shingoni na mikononi.
Nikamkaribia ili nijue alikuwa na nia gani. Kwa bahati mbaya
hatukelewana kimazungumzo na hakuwa tayari kunisikiliza, ikabidi shemasi
amchukue kwenda pembeni ya mkutano. Lakini suala hilo likawa kichwani
mwangu kwa muda mrefu. Mfano mwingine, Sabato moja, niliomba watu walio
na maombi maalumu waje ofisini kwangu baada ya ibada ili tuombe pamoja.
Watu kadhaa walikuja. Mmoja wa waliokuja, alikuwa amempoteza mke wake
kwa kifo mwaka uliokuwa umepita, na kipindi hicho, ndicho kilikuwa
memorial anniversary.
Ilipofika zamu yake alisema, wiki hii nimekuwa nikitafakari kujiua kwa
kumkumbuka mke wangu aliyefariki. Nilishikwa na mshangao mkubwa, ila
nilificha moyoni mwangu kama kiongozi, ili nimpe matumaini na kuomba
naye pamoja na kundi lililokuwa limekuja. Namshukuru Mungu kuwa Mzee
huyo alipata matumaini kwa Bwana Mungu na aliendelea kuishi. Ninapotoa
kisa hiki, ninakumbuka miaka yangu ya kuhudumu kule Texas miaka ya
nyuma, lilikuwa ni kanisa dogo. Baadaye nikahamia State nyingine. Baada
ya muda kadhaa, nikakutana na washiriki wawili kutoka kanisa lile dogo
kule texas. wakanipa taarifa kuwa mama... mama fulani) alijiua. Nikaumia
sana moyoni mwangu. Nikajiuliza, je nilipokuwa kule kuna jambo ambalo
ningemsaidia huyo mama ambalo lingempa tumaini la kuishi. Je, katika
mahubiri au mafundisho yangu ya Biblia, ni jambo gani ambalo ningelitoa
ambalo lingemsaidia hata baada ya miaka kupita lingempa tumaini la
maisha? Je, washiriki na viongozi wa kanisa hilo waliofuata,
wangemsaidiaje huyo mama ili asifikie mahali na kukata tamaa ya kuishi?
Hali
ya kukata tamaa sio ngeni. Tunakumbuka katika Agano la Kale kisa cha
Musa alipotaka Mungu akatishe maisha yake, pia Nabii Eliya alipokuwa
amekimbilia kwenye pango akiwa amekata tamaa ya maisha.
Kwa
viongozi na washiriki wa Kanisa tuna majukumu makubwa, sio tu kwa ajili
yetu wenyewe, bali pia na wale tunaokutana nao NDANI NA PIA NJE YA
KANISA ili kujihimiza na pia kuwahimiza wengine ili kuendelea kuwa na
matumaini kwa Mungu wa mbinguni katika safari ya maisha.
Mchungaji
fulani katika conference fulani Amerika, alielezea kisa hiki kwenye
mkutano wa Makambi: Alipokuwa Mchungaji kijana alitumwa kwenda kanisa
fulani kuwa kiongozi hapo. Mara tu baada ya kufika mshiriki mmoja akaja
kulalamika kuwa mwaka wa 1963 mshiriki mwingine alimtendea jambo baya
sana. Huyu mchungaji kijana akasema, "Ndugu yangu suala hilo liliwatokea
kabla ya mimi kuzaliwa. Sasa unategemeaje mimi nije kulisuluhisha,
baada ya wewe kukaa nalo miaka hii yote na mko kanisa moja? Huyu
mchungaji alitoa kisa hicho kufundisha umuhimu wa msamaha wa kikristo
(forgiveness in Christianity).
Ni
muhimu kusamehe na kuendelea na maisha mbele, La sivyo tukikaa na
mabaya kwa muda mrefu, yanafanya madhara kwetu wenyewe kuliko wale
tunaowakasirikia. Hata kama yule aliyetukosea asirudi kuomba msamaha, au
asikubali kuongea ili kusuluhisha suala na misamaha itokee, jukumu letu
ni kusamehe. Ila haya hayawezekani, isipokuwa kwa maombi na unyenyekevu
tukimruhusu Roho Mtakatifu aendelee kufanya kazi mioyoni na akilini
mwetu.
2)Safari yenye matumaini inahitaji tuwe na imani kwa Bwana Mungu wetu kwa ajili ya mapya.
Katika mafungu ya Isaya hapo juu, Bwana anaahidi kutufanyia kitu na/au mambo mema mapya.
Tunakumbuka
yale Bwana aliyotutendea katika maisha yetu, lakini, tusiishie kwenye
kumbukumbu tu (Memories only). Tumuombe Bwana ili kwa huruma na neema
yake atusaidie tulio viumbe wake tumuone akitenda mapya makuu katika
maisha yetu ya kila siku. Ni rahisi sana yule adui shetani kuleta vurugu
na mawimbi, na giza, ili kujaribu kutuzuia tusione kazi ya Bwana ya
kila siku katika maisha yetu.
Wakati
fulani nilimsikiliza mhubiri aliyekuwa amealikwa kama Guest Speaker,
ambaye alikuwa former, then retired, General Conference Executive
Secretary. Pastor R. akasema kuwa alipokuwa katika uongozi no. 2
Executive position kule GC Headquarter, alichokuwa akisema au kufanya,
in Official Capacity, kilikuwa kinapewa uzito mkubwa unaostahili. Ila
mambo yalibadilika baada ya yeye kutoka hapo ambavyo ni kama kawaida kwa
kila uongozi. Ila akasema kwa kusisitiza, hataki kukaa na kumbukumbu ya
'position' hiyo ya juu tu na kuacha kumfanyia Bwana kazi hali
akiendelea kuishi. Pastor R. alieendelea, "The things we do for the Lord
may not be written in the Adventist Review, other Church Journals, or
even receive, "Thank You Notes" from others, but we must continue to do
them, because we are doing for our Lord and Saviour Jesus Christ and His
people". "Jesus has done a lot more for us. He gave His own life for
our redemption".
3)Safari yenye matumaini inahitaji tumtumaini Bwana kwa ajili ya maisha yetu yajayo.
Yeremia
29:12. "Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni
mawazo ya amani, wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za
mwisho."
Katika
mafungu ya Isaya 43:18-20 Bwana hakuahidi kuondoa misitu wala kuondoa
majangwa katika maisha. Ila Mungu wetu ameahidi kuwa ataweka njia au
barabara njema wakati misitu ikiendelea kuwepo, na ataweka maji mazuri
wakati majangwa yakiendelea kuwepo.
No comments:
Post a Comment