AGAPE SINGERS

Sunday 11 August 2013

IBADA YA MAZISHI YA MAREHEMU PETER HENRY SENDI na Mchungaji Muso

 






Marehemu Peter Henry Sendi

 

Kanisa la Nyasho S.D.A la mjini Musoma limepatwa na majonzi makuu baada ya kuondokewa na mpendwa wao Sendi aliyekuwa.

Marehemu alishiriki kikamilifu katika uhamasishaji wa shughuli za injili za kanisa akihudumu kama mwanachama wa kundi maalumu la ujenzi wa makanisa ya kisabatho ndani na nje ya jimbo la Mara.

Kundi hilo linalojulikama kama "Church Planters" linaoongozwa na Asheri Mukama ambaye ni mkuu wa Idara ya Uwakili kanisa la Kamunyonge limeonyesha juhudi kubwa kufanikisha huduma za neno la Mungu kwa kujitoa katika shughuli hizo za ujenzi na huduma nyingine za uinjilisti.

Akitoa hotuba ya mazishi yaliyofanyika Kanisani Nyasho, Mchungaji Muso amewakumbusha waumini juu ya kumjua Yesu Kristo kama mwokozi wao. Amewahimiza juu ya kumtegemea yeye kama ilivyokuwa kwa mtumishi wa Mungu Lazaro ambaye alikufa kwa matumaini na hivyo kufufuliwa kutoka wafu.


Fungu kuu la Ibada hii ya mazishi limetokakatika kitabu cha   Yohana 11. linalozungumza juu ya kifo cha Lazaro na ufufuo wake kupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Kaimu Mkurugenzi mkuu wa AGS Bwn Fredy Jeje akitoa salamu zake za rambirambi kwa kanisa amemuelezea marehemu sendi kama mtumishi wa Mungu aliyetumia uwezo wake wa Kiuchumi kueneza neno la Mungu. Amewaomba washiriki kujifunza kutoka kwa marehemu kwa kuiga yale yote mema aliyoyatenda ili wahudumu kwa Bwana na kulitangza neno lake kwa watu wote.

"BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA--- JINA LAKE LIHIMIDIWE"
 



No comments: